Ni dhahiri kuwa, katika ulimwengu huu hatuwezi kuishi wala kuwa na ujasiri wa kusimama imara bila nguvu ya kweli kutoka kwa Mungu, hivyo ili kuwa kielelezo bora katika maisha haya chini ya jua inatupasa kumwabudu Mungu wa kweli.

Biblia humsimulia Danieli kama mtumishi mwaminifu wa Mungu katika ufalme wa Babeli. Alitambulika kwa busara yake na imani thabiti katika Mungu. Wapinzani wake walitaka kumwangamiza, hivyo wakampangia njama na kumshawishi Mfalme kuweka amri kwamba kila mtu atakayesali kwa mungu mwingine isipokuwa mfalme, atatupwa katika tundu la simba.

Danieli hakuogopa amri hiyo na aliendelea kumwabudu Mungu wake mara tatu kwa siku, akifungulia dirisha lake kuelekea Yerusalemu. Alipokamatwa na kutupwa kwenye tundu la simba, Mungu alimlinda. Simba hao hawakumdhuru kabisa, na Danieli aliokolewa salama. Mfalme akastaajabishwa na ukuu wa Mungu wa Danieli na akaweka amri nyingine kuwa watu wote walipaswa kumwogopa na kumheshimu Mungu wake Danieli.

UJUMBE WA UKARIBISHO KUTOKA KWA ASKOFU

Karibu Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania. Sisi ni sehemu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato ambayo ni jamii ya watu waliokusudia kwa nia moja, kukuza uhusiano wa karibu kabisa na Mungu wao na kuwa na mwenendo kama aliokuwa nao Yesu. Kiini cha utume wetu ni kuushuhudia ulimwengu juu ya tumaini pekee lenye baraka linalotokana na uzoefu binafsi wa mahusiano bora na Mungu Mwokozi wetu mwenye Upendo, na kujiandaa kwa tukio kubwa kabisa la marejeo yake ambayo yamekaribia sana.